NEW DELHI : Madarzeni wanasa katika ajali ya treni | Habari za Ulimwengu | DW | 02.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW DELHI : Madarzeni wanasa katika ajali ya treni

Madarzeni ya watu mashariki mwa India wamenasa baada ya daraja lililojengwa miaka 140 iliopita kuliangukia behewa moja la treni katika kituo cha reli.

Vyombo vya habari vya India vimeripoti kwamba takriban watu 150 walikuweko ndani ya treni wakati ajali hiyo ilipotokea mapema asubuhi katika kituo cha treni cha Bhagalpur kilioko kilomita 1,240 mashariki mwa mji mkuu wa New Delhi.

Watu 20 wameokolewa na kufikishwa hospitali kutokana na majeraha lakini abiria wengine bado ingali wamekwama kwenye treni hiyo.

Reli ya India mojawapo ya mifumo ya reli ilio mikubwa kabisa duniani husafirisha zaidi ya abiria milioni 13 kila siku na hurepoti takriban ajali 300 kila mwaka.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com