1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW DELHI: Kina cha maji kwenye mito chapungua

7 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbV

Kina cha maji kimeanza kupungua katika mito kadhaa nchini India na Bangladesh baada ya mvua kubwa kusita kunyesha.

Wafanyakazi wa kutoa misaada wamepata fursa ya kufikisha misaada ya dharura kwa wahanga wa mafuriko.

Jimbo la Bihar nchini India ndio lililoathirika zaidi na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa.

Takriban watu 1,500 wameuwawa nchini India, Bangladesh na Nepal kufuatia msimu huu wa mvua na zaidi ya watu milioni 25 wamepoteza makaazi yao.

Watalaamu wa afya wameonya juu ya kuzuka magonjwa yanayo enezwa na maji machafu.