Netanyahu ashikilia msimamo wake | Matukio ya Kisiasa | DW | 24.05.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Netanyahu ashikilia msimamo wake

Waziri Mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu leo ataowainisha mtazamo wake kuhusu mchakato wa amani katika hotuba yake katika bunge la Marekani.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Katika hotuba yake kwa ya kundi la Waisrael lenye ushawishi mkubwa nchini Marekani AIPAC jana jioni mjini Washington, Waziri Mkuu huyo kwa mara nyingine ameapa kutojiondoa katika mpango huo asiyoweza kuutetea na kuilaumu Wapalestina kushindwa kutatua mgogoro bainja yao uliodumu kwa miongo kadhaa sasa.

Netanyahu alisema mgogoro huo hivi sasa unakaribu karne moja kwa sababu Wapalestina wamekuwa wakaidi kuufikisha kikomo, wanakaidi kulikubali taifa la Kiyahudi na kuongeza kwa kusema ingwezekana tu kufanikisha amani miongoni mwao pale ambapo watakubali kufanya mazungumzo na taifa la kiyahudi.

Obama und Netanjahu Treffen Washington

Rais Barack Obama akizungumza na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Kauli hiyo inatolewa wakati ambapo kumekuwa na tofauti ambapo Rais Barack Obama ambae kwa mara ya kwanza alitoa kalui yake hadharini iliyosema taifa la Wapalestina liundwe kwa kuzingatia mipaka iliyokuwepo kabla ya vita vya siku sita vya mwaka 1967.

Taifa hilo litajumuisha Ukanda wa Gaza, Ukingo wa Magharibi na hasa sehemu ya Jerusalem iliyotekwa na Waarabu lakini Israel wamezuia mashariki mwa Jerusalem, kwa marekebisho ili waweze kufanya makazi yao.

Spika wa Bunge la Marekani Jonh Noehner, kutoka chama cha Republican ambae ana dhamira ya kumuondoa Obama katika kinyang'anyiro cha kuwania urais cha 2012 ameuahidi umma wa Israel kwamba atauhakikishia usalama wao kwa asilimia 100.

Ukosoaji pia umetolewa hata upande wa chama cha Obama mwenyewe ambapo Seneta Harry Reid amesema hakuna mtu mwenye uwezo wa kuweka vipimo kuhusu mipaka, majengo na kitu kingine chochote.

Waandamanaji waliingilia kati hotuba ya Netanyau wakisema kukana kuwepo kwa madhila ya Wapalestina ni jambo lisilokubalika lakini upinzani wao uligubikwa na wajumbe wengi waliokuwepo.

Waziri mkuu huyo wa Israel, Netanyahu anatarajiwa kulihutubia Bunge la Marekani wakati huu wa vuta nikuvute kati yake na rais Obama.

Mwandishi: Sudi Mnette AFP

Mhariri:Abdul-rahman

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com