1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ne Muanda arejea nyumbani baada ya kuzuiliwa hospitalini

4 Agosti 2020

Kiongozi wa Kanisa la Bundu dia Mala nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambae pia ni mbunge wa zamani, Ne Muanda Nsemi, tayari amerejea nyumbani kwake baada ya kuzuwiliwa hospitalini kwa muda wa miezi mitatu.

https://p.dw.com/p/3gOhZ
Maafisa wa usalama mbele ya gereza linalodaiwa kuteketezwa moto na wafuasi wa kiongozi wa kidini Ne Muanda Nsemi mnamo 17.05.2017.
Maafisa wa usalama mbele ya gereza linalodaiwa kuteketezwa moto na wafuasi wa kiongozi wa kidini Ne Muanda Nsemi mnamo 17.05.2017.Picha: Reuters/R. Carruba

Ne Muanda alikamatwa mwezi Aprili na kupelekwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa afya ya akili yake, kufuatia mapambano kati ya wafuasi wake na polisi, ambamo watu 14 waliuawa, baada ya kudai kuwa ametumwa na Mungu kuchukuwa madaraka nchini humo.

Zacharie Badiengila, maarufu kwa jina la Ne Muanda Nsemi alikuwa amelazwa hospitalini ‘‘Cliniques universitaires'' hapa mjini Kinshasa, kutokana na ugonjwa wa kichwa ambao ulifwatiwa na ule wa covid-19.

Baada ya kutibiwa kwa muda wa miezi mitatu na kufwatiliwa ipasavyo, Ne Mwanda Nsemi karuhusiwa kurejea nyumbani kwake Macampagne hapa Kinshasa. Makao yake yaliyokuwa yameharibiwa wakati wa mapambano tayari yamekarabatiwa na serikali.

Na kabla ya kuondoka hospitalini Jumatatu, Ne Muanda nsemi alizungumza na waandishi habari akishukuru kwa kushughulikiwa vyema na akasema atawatetea madaktari pia wauguzi.

Soma pia:Juhudi za kusaka utulivu Kivu Kaskazini

"Nitakuwa msemaji wenu ili kuwatetea mahali pote kwani mnafanyakazi nzuri, ila nimesikia mnalipwa vibaya. Nimeona na nitawasemea. Muniamini. Hivi hali yangu tayari imekuwa nzuri, wamekuja kunichukuwa ili nirejee nyumbani kwangu. Ninyi madaktari, nawashukuru kweli." Amesema Ne Muanda Nsemi.

Ne Muanda Nsemi alikuwa sasa anahitajika na kanisa lake la Bundu dia Mayala ambalo pia linatambulika nchini humo kama chama cha kisiasa.

Jamaa zake pia walikuwa wameanza kulalamika na kuomba aruhusiwe kurejea nyumbani ili kupumzika wakidai kuwa amekuwa dhaifu kutokana na kukaa hospitali muda mrefu. Na miongoni mwa waliomsindikiza toka hospitalini hadi makao yake, kuna kiongozi wa kamati ya uchunguzi wa utekelezaji mkataba wa mwaka 201

 Umoja wa Mataifa wachunguza mauaji DRC

Joseph olengankoy kachukuwa fursa ili kuwashukuru wote waliojihusisha na jambo hilo, uhususan rais Felix Tshisekedi kwa yote aliyofanya ili kumuepusha Ne Muanda Nsemi na hatari zote.

Joseph olengankoy amesema: "Hali sasa ni nzuri katika makao yake na ndiyo maana tulikuja kumchukuwa. Tunawashukuru wote waliosaidia kwa njia moja au nyingine. Tunamshukuru sana rais wa taifa kwa kujishughulisha binafsi na kufwatilia kwa makini hali hapa hospitalini na nyumbani."

Tukumbushe kwamba Ne Muanda Nsemi alikuwa ametuhumiwa kwa uasi, kuvuruga usalama wa taifa pia kueneza chuki za kikabila. Lakini wataalam wanasema tuhuma hizo zote zitawekwa kando kwani alitenda bila dhamiri.

Mwandishi: Jean Noel Ba-Mweze, DW, Kinshasa.