Ndege za Kijeshi nchini Kenya zashika doria mpakani mwa Somalia | Matukio ya Kisiasa | DW | 04.06.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Ndege za Kijeshi nchini Kenya zashika doria mpakani mwa Somalia

Nchini Kenya ndege za kijeshi za vita zinaripotiwa kushika doria kwenye eneo linalopakana na Somalia.

Ndege hizo zinashika doria karibu na eneo la Liboi ambako wapiganaji wa Somalia walishambulia kituo kimoja cha polisi mwishoni mwa juma lililopita.Kwa mujibu wa wakaazi wa eneo hilo shambulio hilo lilifanywa na kundi lijulikanalo kama Shabaab ambalo Marekani imeliweka kwenye orodha ya makundi ya kigaidi.

Ili kupata picha halisi katika eneo hilo la mpaka Thelma Mwadzaya amezungumza na Bogita Ongeri afisa wa uhusiano katika Wizara ya Ulinzi nchini Kenya.
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com