Ndege ya Ujerumani yaripuka | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 26.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Ndege ya Ujerumani yaripuka

---

MOSCOW

Ndege moja ndogo ya kibiashara ya Ujerumani imeripuka wakati ikiruka katika uwanja wa ndege wa Almaty nchini Kazakhstan.Abiria pekee aliyekuwa ndani ya ndege hiyo aliuwawa na wafanyikazi watatu wa ndege hiyo walijeruhiwa ingawa abiria aliyekufa haijulikana ni raia wa nchi gani.Rubani pamoja na msaidizi wake wote wajerumani pamoja na mhudumu katika ndege hiyo ambaye ni mturuki walipelekwa hospitali wakiwa na majeraha mabaya.Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa ndege hiyo iligonga ukuta muda mfupi baada ya kuondoka kwenye barabara na hatimaye ikaripuka.Ndege hiyo ilitokea Hannover Ujerumani na ilikuwa imetua kwa muda nchini Kazakhstan kabla ya kuelekea kituo chake cha mwisho Hongkong.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com