Ndege ya Tanzania kuachiwa Afrika Kusini | Matukio ya Afrika | DW | 04.09.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Ndege ya Tanzania kuachiwa Afrika Kusini

Mahakama nchini Afrika Kusini imeruhusu kuachiwa kwa ndege ya shirika la ndege la Tanzania, iliyokuwa imezuwiliwa kwa amri ya mahakama.

Ndege ya shirika la ndege la Tanzania ATCL iliyokuwa imezuiliwa Afrika Kusini inatarajiwa kurejea Dar es salaam wakati wowote baada ya mahakama katika Jimbo la Gauteng kutoa uamuzi wake leo wa kuiruhusu ndege hiyo kuondoka.

Maofisa wa Serikali ya Tanzania wamesema ndege hiyo iliyokuwa imezuiliwa kwa takribani wiki mbili itarejea nyumbani na kuendelea na ratiba zake kama ilivyokuwa awali.

Hata hivyo, Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo la ndege, Ladslausi Matindi amesema bado ilikuwa haijajulikana muda gani ndege hiyo itaondoka katika uwanja wa Oliver Tambo kwa vile shughuli za kukatisha tiketi kwa ajili ya abiria bado ilikuwa haijakamilika.

Pia, amesema maofisa wa shirika hilo wanaendelea kufanya tathmini kujua hasara iliyopatikana tangu ndege hiyo izuiliwe kwa amri ya mahakama.

Kuzuiliwa kwa ndege hiyo kulifuatia maombi yaliyowasilishwa mahakamani na mfanyabiashara mmoja anayeidai serikali ya Tanzania mamilioni ya fedha kama fidia ya kutaifishwa kwa mali zake katika miaka 1980.

Chanzo: George Njogopa