1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi za Afrika magharibi zapinga mkataba mpya wa kiuchumi na Umoja wa Ulaya

Siraj Kalyango5 Desemba 2007

Nchi ya Senegali imekataa kutia sahihi mkataba mpya wa kibiashara kati ya bara la ulaya na nchi za umoja wa Afrika karibi na Pasifiki-yaani ACP.

https://p.dw.com/p/CXYJ
Rais wa Senegal Abdoulaye Wade, asema hatasaini mkataba mpya na ulayaPicha: AP

Kuna juhudi za pamoja kati ya tume ya Ulaya pamoja na nchi 78 za umoja wa ACP,za kupata mikataba mipya ifikapo mwisho wa mwaka wakati mkataba wa sasa wa biashara nafuu utakapo malizika.Kwa mujibu wa duru kutoka Dakar, mji mkuu wa Senegali,rais wa nchi hiyo, Abdoulaye Wade anasemekana kugoma kutia sahihi mkataba mpya unaopendekezwa na tume ya Ulaya.

Hata hivyo sio tu Senegal iliokataa lakini pia kuna nchi zingine za umoja wa ACP nazo zimetishia kuugomea.Bw Wade ametoa sababu kuwa,mpango huo unapingwa na jumuia ya kiuchumi ya nchi za Afrika magharibi-ya ECOWAS.

Mapema mwezi jana, nchi 15 zinazouunda umoja wa ECOWAS, zilitangaza utayarifu wao wa kutotia dole hati hiyo zikidai kuwa hali zilizomo sasa haiwaruhusu.

Rais Wade amefafanua kuwa kutokana hali hiyo,Umoja wa Ulaya,sasa unazitaka nchi binafsi kutilia sahihi mkataba huo.

Umoja wa ulaya unasema kwa upande wake kuwa umesha pata maelewano fulani na nchi za Botswana, Lesotho, Swaziland pamoja na Msumbiji.

Hata hivyo,mkataba wenyewe unaopendekezwa umesha kataliwa na nchi kadhaa pamoja na mashirika ya kimataifa, kwa hofu ya athari kwa nchi maskini za umoja wa ACP.

Mikataba mipya itazitaka nchi za ACP, kufungua milango yake kwa bidhaa za Ulaya.Nazo nchi hizo zinaahidiwa kufaidika kwa kupewa ruhusa kupenya soko la ulaya kuanzia januari mosi mwaka ujao.

Hata hivyo bidhaa za mchele na sukari hazimo katika maelewano hayo.

Mikataba iliko kwa sasa ,ya soko nafuu kwa masoko ya wakoloni wazamani, ni lazima ibadilishwe ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Shirika la biashara duniani-WTO-linasema mikaba hiyo si halali.

Wakati Senegali ikipinga kusaini mkataba huo,Sierra Leone kwa upande wake, inasema iko tayari kuukubali.

Waziri mdogo wa Fedha wa Sierra Leone, Richard Conteh,amesema kuwa nchi yake itafanya hivyo kwa sababu haitaki kuachwa nyuma.

Aidha amesema kuwa serikali za nchi ambazo ni za pili kwa umaskini duniani, zimechukua aliouita , ‘msimamo thabiti’ kuelekea suala hilo.