Nawaz Sharif azuiwa kugombea. | Habari za Ulimwengu | DW | 03.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Nawaz Sharif azuiwa kugombea.

Islamabad. Tume ya uchaguzi nchini Pakistan imemzuwia waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo na kiongozi wa chama cha upinzani Nawaz Sharif kutogombea uchaguzi utakaofanyika hapo Januari 8. Maafisa wamesema kuwa hii ni kutokana na hukumu iliyotolewa dhidi ya Sharif katika madai ya utekaji nyara mwaka 2000 kuwa ndio sababu ya kukataliwa kwa fomu zake za uteuzi.

Kesi hiyo inamhusisha jaribio la Sharif kutaka kuzuwia ndege ambayo ilikuwa inamemchukua mkuu wake wa jeshi wa wakati huo Pervez Musharraf , kutua nchini Pakistan mwezi Oktoba 1999. Musharraf na jeshi la nchi hiyo walimuondoa madarakani Sharif kutokana na tukio hilo. Sharif aliwasili mjini Islamabad mapema jana kwa mazungumzo na kiongozi mwingine wa upinzani waziri mkuu wa zamani Benazir Bhutto, kuhusu mipango ya kuususia uchaguzi huo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com