NATO yatiwa hasara tena. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 09.10.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

NATO yatiwa hasara tena.

Malori ya Nato ya kusafirishia mafuta yashambuliwa tena nchini Pakistan.

Magari ya matanki ya mafuta yakiwaka moto baada ya kushambuliwa na wapinzani.

Magari ya matanki ya mafuta yakiwaka moto baada ya kushambuliwa na wapinzani.

ISLAMBAD:

Malori ya mafuta takriban 30 ya majeshi ya Nato yameshambuliwa nchini Pakistan.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi shambulio hilo lilifanyika katika jimbo la Baluchistan kusini magharibi mwa Pakistan. Msafara huo wa malori ulikuwa upeleke mahitaji kwa ajili ya majeshi ya kimataifa yaliyopo nchini Afghanistan.

Majeshi ya Nato yanalazimika kutumia njia ya kusini magharibi mwa Pakistan kwa sababu Pakistan imeifunga njia iliyopo kwenye mpaka wake muhimu kufuatia mkwaruzano na Marekani

Polisi wawili pia walijeruhiwa katika shambuli hilo.Taarifa ya serikali imesema kwamba washambuliaji wapatao 10 walitumia bunduki na roketi kuyateketeza malori hayo ya kusafirishia mafuta yaliyokuwa yameegeshwa njiani karibu na mkahawa.

Shambulio hilo nila sita kufanyika mnamo muda wa wiki moja.

 • Tarehe 09.10.2010
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Pa4L
 • Tarehe 09.10.2010
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Pa4L
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com