1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO yashinikiza msaada kwa Afghanistan

15 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cbxp

EDINBURGH

Nchi zenye wanajeshi wanaopigana nchini Afghanistan zimekubaliana kubuni njia mpya za kuituliza nchi hiyo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Mawaziri ktuoka nchi nane wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya Mataifa ya Magharibi NATO wamekutana huko Endiburgh Uingereza wakati wasi wasi ukiongezeka juu ya mapungufu ya kikosi cha Kimataifa cha Usaidizi wa Usalama ISAF cha wanajeshi 40,000 kinachoongozwa na NATO pamoja na kuongezeka kwa uasi wa kundi la Taliban.

Uingereza na Marekani zimekuwa zikitowa wito mara kwa mara kuzitaka nchi nyengine kutowa mchango wao zaidi katika mapambano dhidi ya Taliban.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Robert Gates pia amesema kwamba nchi wanachama wa NATO zitatafuta njia nyengine za kutowa michango badala ya kutowa wanajeshi zaidi.