NATO yakubali kuondoa majeshi Afghanistan 2014 | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 20.11.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

NATO yakubali kuondoa majeshi Afghanistan 2014

Ingawa NATO imetoa ratiba hiyo ya 2014 kumaliza operesheni za kijeshi, afisa wa ngazi ya juu wa Marekani asema wao bado hawajaamua.

default

Katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen akiwa Lisbon

Rais wa Urusi Dmitry Medvedev amewasili mjini Lisbon, Ureno kwa mazungumzo kuhusiana na mfumo wa ulinzi wa pamoja wa makombora ya kujihami pamoja na mkakati wa vita nchini Afghanistan. Huu ndio mkutano wa kwanza kati ya Jumuiya ya Mataifa ya Magharibi NATO na Urusi katika miaka miwili. Mapema viongozi wa Jumuiya hiyo wanaohudhuria mkutano huo wa siku mbili walikubaliana kuanza kuyaondoa majeshi yao Afghanistan kuanzia mwaka ujao, lakini wakaapa kwamba hawatoiacha serikali ya Afghanistan kulemewa na kundi la Taliban ambalo bado ni kitisho.

NATO Gipfel Portugal Lissabon November 2010

Rais Hamid Karzai wa Afghanistan.

Mataifa hayo 48 ambayo yana majeshi yao Afghanistan walisaini mkataba na rais Hamid Karzai kuyapa majeshi ya Afghanistan jukumu la usalama wa nchi yao kuanzia mwaka ujao 2011 na kuondoka kabisa 2014. Katibu Mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen alisema Jumuiya hiyo bado itaiunga mkono Afghanistan hata baada ya kumalizika rasmi kwa opereshini za mapigano.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com