NATO yaidhinisha mkakati mpya wa ulinzi | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 22.11.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

NATO yaidhinisha mkakati mpya wa ulinzi

Merkel aipongeza Urusi kwa kushiriki mkutano wa NATO, huku Urusi nayo ikitaka fursa kamili ya kuwa mshiriki wa mikakati ya ulinzi dhidi ya makombora na sio msindikizaji tu

default

Katibu mkuu wa NATO Jenerali Anders Fogh Rasmussen akihutubia mkutano mjini Lisbon.

Katika mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa Shirika la Kujihami la NATO uliofanyika mjini Lisbon, Ureno, viongozi hao wameidhinisha mpango mpya wa miaka 10 ijayo unaoliruhusu Shirika hilo kupambana na vitisho vipya vya ugaidi.

Hii ni pamoja na uvamizi wa mitandao. Mipango ya kuunda mfumo wa pamoja wa ulinzi na Urusi, pia ilijadiliwa. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameutaja mkutano huo wa NATO kama nafasi muhimu katika uhusiano kati ya mataifa ya Mashariki na Magharibi. Hii ni mara ya kwanza kwa Urusi kushiriki katika mkutano huo wa NATO.

Mwandishi: Maryam Abdalla/DPAE, Reuters

Mhariri: Sekione Kitojo

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com