Namibia na Ujerumani zavutana kuhusu fidia | Matukio ya Afrika | DW | 23.03.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Namibia na Ujerumani zavutana kuhusu fidia

Ni katika mazungumzo juu ya fidia ambayo Ujerumani inapaswa kuilipa Namibia kuhusiana na mauaji ya kimbari yaliyofanywa na wanajeshi wa Ujerumani dhidi ya Wanama na Waherero wa Namibia kati ya mwaka 1904 na 1908,

Kiongozi wa ujumbe huo Ruprecht Polenz amesema kiasi kinachodaiwa na Namibia ni kikubwa mno, kuliko ambacho Ujerumani inaweza kukitoa. Ameliambia shirika la habari la Ujerumani kuwa juu ya msaada wa kimaendeleo kwa Namibia, Ujerumani pia iko tayari kuongeza kiwango kingine ambacho hata hivyo hakikutajwa wazi. Ujerumani na Namibia zimekuwa zikijadiliana kwa miaka mitatu sasa juu ya fidia hiyo, na Polenz ameeleza kuwa duru nyingine ya majadilino inatarajiwa mnamo wiki chache zijazo. Mwanzoni mwa karne ya 20, wanajeshi wa Ujerumani waliuwa maelfu na maelfu ya Wanama na Waherero wa Namibia, ambayo wakati huo ilijulikana kama Ujerumani ya Kusini Magharibi mwa Afrika. Kuanzia mwaka 2015, Ujerumani imekuwa ikiyatambua rasmi mauaji hayo kuwa ya kimbari.