1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Wasomalia wakubaliana

8 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBb5

Wajumbe waliyokuwa wakihudhuria mkutano wa maridhiano ya kitaifa nchini Somalia wametia saini makubaliano ya kusitisha mapigano.

Hata hivyo mkutano huo haukuudhuriwa na ujumbe wa wanamgambo wa kiislam ambao wamekuwa wakiendesha vita vya msituni.

Balozi wa Somalia nchini Kenya Mohamed Ali Nur amesema kuwa wajumbe zaidi ya 2,000 waliyokutana mjini Nairobi Kenya wiki iliyopita walitia saini makubaliano hayo ambayo utekelezaji wake ulitegemewa kuanza toka tarehe mosi mwezi huu.

Hata hivyo hakusema ni vipi makubaliano hayo yatafanyakazi.