NAIROBI:Wakazi wa Mathare wakimbia makazi yao | Habari za Ulimwengu | DW | 08.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI:Wakazi wa Mathare wakimbia makazi yao

Wakazi wa mtaa wa mabanda wa Mathare wanaripotiwa kutoroka makazi yao baada ya ghasia na misako ya polisi kuwasaka wafuasi wa kundi lililopigwa marufuku la mungiki.Kundi hilo linadaiwa kutekeleza mauaji ya zaidi ya watu 30 wiki hii.Wengi ya wakazi hao walionekana wakibeba vitu vyao vya matumizi ya nyumbani na kuvipakia katika malori au kujitweka vichwani.

Polisi wamewauwa zaidi ya watu 30 tangu mwanzoni mwa wiki hii walioshukiwa kuwa wanachama wa kundi hilo la Mungiki na kuwakamata wengine 300 katika mtaa wa mabanda wa Mathare.Mtaa huo unaaminika kuwa ngome ya kundi la Mungiki.Maafisa hao wa usalama walipata bunduki tatu na vipande vya miili ya binadamu vinavyodhaniwa kutumika katika shughuli za siri za kundi hilo.

Kundi la Mungiki linalaumiwa kusababisha vifo vya yapata watu 20 katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita ikiwemo miili ya watu 12 iliyokatwakatwa au kuchinjwa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com