1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Waangalizi wa kigeni kushiriki katika uchaguzi wa Disemba

9 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C78k

Kenya inawaalika waangalizi wa kigeni nchini mwake huku uchaguzi mkuu ukisubiriwa kufanyika tarehe 27 mwezi Disemba.Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ,ECK,Saamuel Kivuitu waangalizi kutoka Umoja wa Afrika,Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya madola ya Commonwealth wanaalikwa kushiriki katika uchaguzi mwishoni mwa mwaka huu.

Balozi wa Uingereza nchini Kenya Adam Woods anatoa wito kwa tume hiyo kutimiza jukumu lake la kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kukiwa na uhuru na haki.Vyama vya upinzani tayari vinalaumu serikali kwa kujaribu kutia ila katika uchaguzi ujao huku tume ya uchaguzi ikisisitiza kutimiza wajibu wake.

Kulingana na kura za maoni mwakilishi wa chama cha ODM Raila Odinga huenda akampiku Rais Kibaki wa chama cha PNU.