NAIROBI:Uchaguzi wa Kenya kufanyika tarehe 27 Desemba | Habari za Ulimwengu | DW | 26.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI:Uchaguzi wa Kenya kufanyika tarehe 27 Desemba

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Kenya Samuel Kivuitu ameitangaza tarehe 27 mwezi Desemba kuwa ndio siku ya kufanyika uchaguzi mkuu nchini humo.

Rais Mwai Kibaki anagombea awamu ya pili ya kipindi cha miaka mitano ya uongozi.

Matukio ya kura ya maoni ya hivi punde hata hivyo yanaonyesha kuwa rais Kibaki amepoteza aumaarufu wake na anamfuata mpinzani wa chama cha ODM bwana Raila Odinga.

Kura ya maoni iliyofanywa na kampuni ya kukusanya maoni ya Steadman inaonyesha kuwa Raila Odinga anaongoza kwa asilimia 53 ilihali rais Kibaki ana asilimia 37.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com