1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Familia ya mtuhumiwa wa ugaidi yalalamika

28 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCEn

Familia ya mshukiwa wa ugaidi wa kundi la Al Qaeda aliyehusika katika shambulio la bomu la mwaka 2002 kwenye hoteli ya Paradise katika mtaa wa Kikambala mjini Mombasa wanasema kuwa hatua ya kumpeleka katika jela ya Guantanamo Bay nchini Cuba si haki.Abdul Malik mshukiwa wa kwanza wa ugaidi kuhamishwa jela ya Guantanamo tangu mwezi Septemba mwaka 2004.

Kwa mujibu wa dadake kwa jina Mariam,ingekuwa sawa kwa yeye kufikishwa mahakamani nchini Kenya kabla kupelekwa Guantanamo Bay.Kulingana na msemaji wa Wizara ya ulinzi ya marekani Pentagon,Malik alikiri kuhusika na shambulio la mwaka 2002 dhidi ya hoteli ya Paradise kwenye mtaa wa Kikambala.Watu 13 walipoteza maisha yao katika shambulio hilo.Aidha anakiri kuhusika na jaribio la kudengua ndege ya abiria ya Israeli iliyokuwa na abiria 271.Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri hadi nchini Kenya.