NAIROBI: Wafanyakazi wa Umoja wa mataifa waondoka kutoka Somalia | Habari za Ulimwengu | DW | 13.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI: Wafanyakazi wa Umoja wa mataifa waondoka kutoka Somalia

Umoja wa mataifa umewaondoa wafanyakazi wake kwa muda kutoka Somalia kufuatia vitisho vya kuuawa. Maafisa wa Umoja wa mataifa mjini Nairobi nchini Kenya, hawakusema ni nani ametoa vitisho hivyo lakini wamesema wanavizingatia kwa makini. Wapiganaji wa muungano wa makundi ya waislamu sasa wanalidhibiti eneo la kusini mwa Somalia ukiwemo mji mkuu Mogadishu na serikali ya mpito ya rais Abdullahi Yussufu inaonekana kuwa dhaifu kuweza kudhibiti hali ya mambo Somalia.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com