Nairobi. Rais wa Somalia aomba msaada. | Habari za Ulimwengu | DW | 20.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Nairobi. Rais wa Somalia aomba msaada.

Rais wa serikali ya mpito ya Somalia ametoa wito jana kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia kupambana na kundi lenye nguvu la Waislamu ambalo amelishutumu kwa kufanyakazi kwa kificho chini ya bendera ya Al – Qaida na Taliban.

Akizungumza katika mji mkuu wa Kenya , Nairobi mbele ya jopo la wanadiplomasia linaloungwa mkono na Marekani , linalojaribu kuokoa mazungumzo yanayolega lega kati ya pande hizo mbili, rais Abdullahi Yusuf Ahmed amesema dunia inawajibu wa kiroho kusaidia kuilinda serikali yake dhaifu dhidi ya magaidi kutoka nje.

Amesema kuwa Waislamu hao ambao wamechukua udhibiti wa mji mkuu wa Somalia , Mogadishu na karibu eneo lote la kusini na kati ya nchi hiyo, wanajifanya kuwa wenye msimamo wa kati na wanaleta kitisho kikubwa katika eneo hilo pamoja na kimataifa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com