NAIROBI: Mkenya ajipeleka kuhojiwa na polisi | Habari za Ulimwengu | DW | 17.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI: Mkenya ajipeleka kuhojiwa na polisi

Raia wa Kenya ambae picha yake ilisambazwa na wachunguzi kuhusika na mripuko uliotokea mji mkuu wa Kenya Nairobi amejipeleka kwa polisi ili apate kuhojiwa.Wachunguzi walisambaza picha ya Farah Ahmed Hirsi mwenye umri wa miaka 41,wakisema ana habari zinazokuhusika na mripuko ulioua mtu mmoja na kujeruhi wengine 37.Hirsi,alikwenda makao makuu ya polisi akifuatana na wakili wake Ahmed Nasser Abdullahi na vile vile kikundi kidogo cha wanaharakati wanaogombea haki za binadamu. Abdullahi amesema,Hirsi hana hatia.Polisi bado hawakuweza kuthibitisha lengo la shambulio hilo au ni kitu gani hasa kilichosababisha mripuko wenyewe.Hakuna ye yote aliechukua dhamana ya mripuko huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com