1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi. Kibaki akataa ongezeko la mshahara.

14 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjd

Rais wa Kenya Mwai Kibaki amekataa jana kuongezwa mshahara karibu mara tatu hatua ambayo ilizusha upinzani katika nchi hiyo ya Afrika mashariki ambapo watu wengi wanaishi kwa pato la chini ya dola moja kwa siku na ulaji rushwa umekithiri.

Bunge lilimpatia rais Kibaki ongezeko la mshahara la asilimia 186, ambalo lingemfanya kuwa mmoja kati ya viongozi wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi katika Afrika na mwenye pato kubwa zaidi kuliko wengi wa viongozi wa mataifa ya magharibi.

Kama ongezeko hilo lingetekelezwa mshahara wa mwezi wa Kibaki ungefikia kiasi cha karibu dola 30,000 kwa mwezi akiwa pia na marupurupu ya dola 18,600.