1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Kamata kamata ikiendelea-wakazi wakimbia Muthare

9 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtO

Nchini Kenya,mamia ya watu wamekikimbia kitongoji cha Mathare ukingoni mwa mji mkuu Nairobi ambako hadi watu 33 wamepoteza maisha yao,huku polisi wakiendelea kuwasaka wafuasi wa kundi la Mungiki. Siku ya Alkhamisi,kama askari polisi 500, waliingia katika kitongoji hicho na kuwapiga risasi na kuwaua si chini ya watu 11 na wakabomoa vibanda na kuwapiga watu,baada ya maafisa 2 kuuawa na kundi la uhalifu la Mungiki hapo siku ya Jumatatu.Polisi nao siku ya Jumanne,waliwaua watu 22.Kwa mujibu wa polisi,watu hao wameshukiwa kuhusika na Mungiki na walikataa kukamatwa.