Nahodha wa Fiorentina afariki dunia | Michezo | DW | 05.03.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Nahodha wa Fiorentina afariki dunia

Nahodha wa Fiorentina na mchezaji wa timu ya taifa ya Italia amefariki dunia baada ya kuugua kwa ghafla

Italien AC Florenz Davide Astori (Imago/ZUMA Press/G. Maffia)

Davide Astori

 

Tuanze  na  tanzia:  Nahodha wa  klabu ya  Fiorentina  na  mchezaji wa  timu  ya  taif  ya  Italia  Davide Astori  amefariki  kutoka  na ugonjwa  wa ghafla akiwa  na  umri  wa miaka 31 jana  Jumapili , na kuliacha  soka  la  Italia  katika  mshituko  mkubwa.

Ligi  ya  Serie A  iliahirisha  michezo  yote ya  jana , ikiwa  ni  pamoja na  pambano  la  watani  wa  jadi  kati  ya  AC Milan na  Inter Milan, wakati  vilabu  vya  Italia  na  Ulaya  kwa  jumla  na  wachezaji kadhaa  walituma  salamu  zao  za  rambi  rambi  na  kueleza mshangao  wao  kwa  kifo  hicho  cha  ghafla. Mlinzi Astori , akiwa katika  msimu  wake  wa  10  katika  Serie A, alikutwa  amefariki katika  chumba  alichopanga  hotelini  mjini  Udine, ambako Fiorentina  ilikuwa  ipambane  na  Udinese katika  uwanja  wa  Dacia Arena  jana  Jumapili. Astori, ambaye  ameshiriki  michezo 298 katika Serie A , alijiunga  na  Fiorentina kwa  mkopo mwezi  Agosti mwaka 2015 na  klabu  hiyo  ilimsaini moja  kwa  moja  mwaka  mmoja baadaye. Aliichezea  Cagliari kwa  misimu  sita  na  mwaka  mmoja kwa  mkopo  katika  klabu  ya  AS roma.  Mungu aieweke  roho  ya marehemu mahali  pema , ameen.

Mwandishi: Sekione  Kitojo /  dpae / rtre / afpe
Mhariri: Yusuf Saumu