Nagelsmann: Bayern wana nafasi nzuri msimu ujao | Michezo | DW | 15.07.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Nagelsmann: Bayern wana nafasi nzuri msimu ujao

Timu za ligi kuu za kandanda Ulaya zinaendelea na maandalizi ya kabla ya msimu mpya na hapa Ujerumani, Kocha mpya wa RB Leipzig Julian Nagelsmann amewataja Bayern Munich kuwa na nafasi nzuri zaidi kuhifadhi ubingwa wao

Lakini ameitaka timu yake kuwa tayari kuyatumia vyema madhaifu yoyote yatakayojitokeza kwa upande wa Bayern.

Nagelsmann, aliyejiunga na Leipzig akitokea Hoffenheim, ameliambia gazeti la Ujerumani la Bild am Sonntag kuwa timu yake changa ya Leipzig bado ina hamu kubwa ya mafanikio katika msimu wake ujao wa nne kaktika ligi kuu ya Bundesliga.

Munich wameshinda mataji saba ya Bundesliga mfululizo lakini msimu uliopita walimaliza mbele za Borussia Dortmund na pengo la pointi mbili tu.

Leipzig walimaliza katika nafasi ya pili, sita na tatu katika misimu yao mitatu ya kwanza, na wakafika fainali ya Kombe la Ujerumani ambapo walipoteza dhidi ya Munich.