Nadal kupambana na Thiem robo fainali | Michezo | DW | 27.01.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Nadal kupambana na Thiem robo fainali

Katika mchezo wa Tennis kuna kipute cha Australian Open kinachoendelea huko Australia ambapo mchezaji nambari moja duniani Rafael Nadal amefuzu robo fainali.

Hii ni baada ya kumbwaga Nick Kyrgios mapema Jumatatu.

Nadal ameshinda kwa seti nne za 6-3 3-6 7-6 7-6 na sasa atapambana na Dominic Thiem.

Baada ya kushinda mechi yake Thiem alikuwa na haya ya kusema.

"Nafikiri nimecheza mchezo wangu bora kabisa. Nina furaha sana kwasababu nimefuzu robo fainali kwa mara ya kwanza hapa Australia," alisema Thiem.