1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Münterfering azungumzia uwezekano wa kushirikiana na Die Linke katika daraja ya kimkoa

Oumilkher Hamidou22 Desemba 2008
https://p.dw.com/p/GLDu
Mkuu wa chama cha SPD F.Münterfering na waziri wa mambo ya nchi za nje F.W. SteinemeierPicha: AP



Mzozo wa kiuchumi haujazuwia biashara isinawiri wakati huu wa X-Mas,Serikali ya muungano pamoja na chama cha mrengo wa shoto Die Linke,inawezekana majimboni anasema Franz Münterfering na  sauti zinaanza upya kupazwa kutaka chama cha siasa kali za mrengo wa kulia NPD kipigwe marufuku.Hizo ni miongoni mwa mada zilizochambuliwa magazetini hii leo.


Tunaanzia na matamshi yaliyotolewa na Franik Münterfering kuhusu uwezekano wa kuundwa serikali ya muungano katika daraja ya kimkoa.Gazeti la Flensburger Tageblatt linaandika:



Ni sawa na tamaa ya kutaka madaraka,pale mkuu wa chama cha SPD  anapoashiria uwezekano wa kuundwa serikali ya muungano hata kati ya chama chake na kile cha FDP.Muongozo wa chama hicho cha kiliberali haulingani hata kidogo na ule ,wa chama cha mrengo wa shoto-Die Linke.Kisebu sebu cha SPD, mara kuzungumzia uwezekano wa kuundwa serikali ya muungano pamoja na chama cha mrengo wa shoto Die Linke na walinzi wa mazingira-na mara nyengine kuhusu muungano kati yao na waliberali  pamaoja pia na walinzi wa mazingira,bila ya kuachana na uwezekano wa kuendelea na serikali ya muungano wa vyama vikuu,kinatoa picha ya jinsi chama hicho kilivyogawika."


Gazeti la Neue Presse la mjini Hannover linaandika


Hofu kuelekea serikali ya nyekundu kwa nyekundu?Muhimu tunaunda serikali tuu:hivyo ndivyo mtu anavyoweza kutathmini matamshi ya Franz Münterfering.Bila ya shaka anazungumzia uwezekano tuu.Hessen imebainisha katika chama cha SPD daima kumekua na wababe ambao mwanya wa kinadharia unaowatenganisha na kambi ya mrengo wa shoto hauwatishi,ikiwa kwa msaada wa kambi hiyo wanaweza kufika madarakani.Hata katika daraja ya shirikisho fikra kama hiyo inaweza kuzuka,japo kama viongozi wa SPD wanaendelea kukana "kamwe haitatokea."Hakuna lakini anaewaamini.


Kuhusu heka heka za X-Mas na mzozo wa kiuchumi,linaandika gazeti la Nordsee-Zeitung la mjini Bremerhaven.


Watu wanamiminika madukani katika kila sehemu ya Ujerumani,kununua zawadi,bila ya kujali mzozo wa kiuchumi.Angalao habari za kutia moyo hizo.Lakini tusihadaike.Wengi bado hawajaanza kuyaona madhara ya mzozo wa kiuchumi ,lakini hali katika viwanda vya magari haiashirii mema.Ndio maana hatua zitakazopitishwa mjini Berlin wiki zijazo,zinapewa umuhimu mkubwa.Hata kama watu hawataki kusikia,mwaka 2009 unatazamiwa kuwa wa shida-kila siku si X-Mas.



Gazeti la Recklinghäuser Zeitung  linaandika


Kujinunulia zawadi,naiwe kwasababu ya sherehe au hivi hivi,ni miongoni mwa hatua za kuupiga jeki uchumi.Jenginelo litazidisha makali ya mzozo ulioko.Serikali inatakiwa ifikirie pia uwezekano wa kuzidisha mishahara ya wafanyakazti kwa namna ambayo kiu cha kununua kitaendelea kupunguza makali ya mzozo wa kiuchumi,na mwakani pia.