Mzozo wa Ukraine Wazidi Makali | Matukio ya Kisiasa | DW | 06.05.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mzozo wa Ukraine Wazidi Makali

Sauti zinazidi kupazwa kutahadharisha dhidi ya kuripuka vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Ukraine.Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi,Ukraine na Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kukutana mjini Vienna.

default

Tawi la Benki lahujumiwa na mali kuporwa huko Donetsk

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza William Hague ,mara baada ya kuwasili mjini Vienna kuhudhuria mkutano wa baraza la Ulaya utakaomulika mgogoro wa Ukraine,ameituhumu Urusi kujaribu kuvuruga uchaguzi wa rais nchini Ukraine.Akizungumza na waandishi habari waziri Hague amesema anataraji "risala kali itatolewa na nyingi kati ya nchi zinazohudhuria mkutano huo, kutaka uchaguzi wa rais uitishwe kama ilivyopangwa."Wananchi wa Ukraine wana haki ya kuwa na serikali yao,rais wao na kuitisha uchaguzi huru na wa kidemokrasia amesema."

Uchaguzi wa rais umepangwa kuitishwa May 25 mwaka huu lakini Moscow imeutaja uchaguzi huo kuwa "hauna maana" huku wanamgambo wananaotaka kujitenga eneo la mashariki wakijiandaa kuitisha kura ya maoni ya kudai uhuru jumapili ijayo.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi Sergei Lavrov hajasema lolote alipowasili Vienna kuhudhuria mkutano huo,wazirio mwenzake lakini wa Ukraine Andriy Deshchytsia amesema:"Tumekuja ili kusaka njia ya kujikwamua toka hali hii iliyoko hivi sasa na kubuni utaratibu utakaotuliza hali ya mambo nchini Ukraine."

Uwezekano wa mafahali wawili kukutana Vienna

Europarat Wien 2014 6.5.14 Außenminister Treffen Ukraine Andriy Deshchytsia Andre Deshchitsa

Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Ukraine Andriy Deshchytsia alipowasili Vienna kuhudhuria mkutano wa baraza la ulaya

Bado si dhahir kama wanasiasa hao wawili waliohudhuria karamu ya chakula cha usiku pamoja na mawaziri wenzao jana usiku mjini Vienna,watakuwa na mkutano baidi pembezoni mwa mkutano huu wa Vienna.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya Austria alisema mjini Vienna mawaziri Lavrov na Deshtschytsia walikutana kwa muda mfupi,lakini hawakuwa peke yao.

Wakati huo huo Urusi imeongeza idadi ya manuari zake na nyambizi katika eneo la bahari nyeusi,kufuatia kile waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu alichonukuliwa akisema "kumezwa raas ya Crimea.

Vikosi vyaangani na nchi kavu navyo pia vitapelekwa katika vituo vya kijeshi vya Urusi katika bahari nyeusi.

Kitisho cha kuripuka vita vya wenyewe kwa wenyewe

Außenminister Treffen in Genf 17.04.2014

Mkutano wa mawaziri wa Mambo ya nchi za nje wa Urusi,Ukraine,Marekani na mwakilishi mkuu wa siasa ya nje ya Umoja wa Ulaya uliofanyika Geneva April 17 mwaka huu

Na nchini Ukraine kwenyewe idadi ya wahanga wa opereshini za kijeshi dhidi ya mji unaodhibitiwa na waasi wa Slavyansk,mashariki ya Ukraine imeongezeka na kufikia watu 34.Kiwanja cha ndege cha Donetsk kimefuingwa-hakuna sababu zilizotolewa.

Sauti zinazidi kutolewa kuonya dhidi ya balaa la kuripuka vita vya wenyewe kwa wenyewe.Kuna hofu rais Vladmir Putin asije akaamuru wanajeshi wake waivaamie nchi hiyo jirani.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters/AFP/AP

Mhariri:Yusuf Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com