1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo wa nuklia wa Korea Kaskazini wachukua mkondo mpya

Thelma Mwadzaya27 Machi 2009

Marekani,Japan na Korea Kusini wanakutana mjini Washington hii leo ili kujadili mivutano inayoongezeka kati ya Korea Kusini na Kaskazini

https://p.dw.com/p/HKca
Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Il akiwa na viongozi wa serikaliPicha: AP



Wapatanishi wangazi za juu kutoka .Kikao hicho kinafanyika baada ya Korea Kaskazini kukaidi onyo za jamii ya kimataifa za kutofyatua kombora la masafa marefu.

Wakati huohuo jehi la wanamaji la Marekani limepeleka manowari mbili kwenye pwani ya Japan zilizo na uwezo wa kufatilia safari za makombora.Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Korea Kaskazini kutangaza kuwa juhudi zozote za kuishtaki kwa Umoja wa Mataifa zinaashiria uchokozi na huenda zikakwamisha mazungumzo ya pande sita yanayolenga kutatua mzozo huo wa nuklia.

Kwa upande mwengine Japan imeliamuru jeshi lake kujiandaa kupambana na vipande vyovyote vitakavyodondoka endapo matatizo yatatokea wakati kombora hilo litafyatuliwa na Korea Kaskazini.

Kwa mujibu wa katiba ya Japan nchi hiyo hairuhusiwi kuingilia kombora lolote iwapo linaelekea sehemu nyengine.Korea kaskazini imetangaza kuwa itafyatua kombora kwa lengo la kufikia anga za mbali kwa satellite ifikapo mwezi ujao kati ya tarehe 4 na 8.

Mwandishi:Thelma Mwadzaya AFPE