1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Federica Mogherini aitaka China izingatie majukumu yake

Admin.WagnerD20 Aprili 2017

Mkuu wa sera ya nje wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini amesema China na Ulaya wana jukumu na maslahi ya pamoja ya kuepusha vita kwenye rasi ya Korea.

https://p.dw.com/p/2bc0W
China EU-Außenvertretterin Federica Mogherini in Pekin
mkuu wa sera ya nje wa Umoja wa Ulaya Federica MogheriniPicha: picture-alliance/AP Photo/M. Schiefelbein

Katika hutuba yake siku ya Alhamisi kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu katika siku yake ya mwisho ya ziara yake mjini Beijing, Mogherini amesema mgogoro na Korea Kaskazini unaweza kuwa  na athari za kimataifa.

Federica Mogherini alisema kuwa China na Umoja wa Ulaya wana maslahi  na majukumu  ya pamoja ya kuhakikisha  Korea ya Kaskazini inatimiza wajibu wake kimataifa na pia inatakiwa kujihusisha na jumuiya ya kimataifa.

Katika hutuba yake huko katika  chuo kikuu cha Tsinghua, Mogherini alionya kuwa mgogoro katika rasi ya Korea unaweza ukaleta matatizo duniani kote.

"Kila mtu anajua kuwa mgogoro wa Korea ya Kaskazini, unaweza kuleta mtafaruku mkubwa duniani," Mogherini aliwaambia wanafunzi wa chuo kikuu hicho ambacho tayari kimetoa viongozi wengi wa China.

Mogherini alisema pia kauli ya mwanawe mwenye umri wa miaka 12, inayosema kuwa China iko katika sehemu inayotishiwa na vita vya silaha za nyuklia, imemuonesha yeye kama kuna hitilafu katika kuwepo nguvu za pamoja za kukabiliana na kupinga mgogoro huo usiendelee.

"Ikiwa mtoto wa miaka 12 anafahamu hatari za kuwepo mgogoro huo, mbali na makaazi yake, huo ni ushahidi wa wazi kuwa sisi tuna jukumu la pamoja la kuzuwia mgogoro huu," alisema Mogherini.

Korea ya Kaskazini na Silaha za Nyuklia

Nordkorea Fernsehübertragung der Militärparade in Pjöngjang
Gwaride ninalooyesha silaha za makombora huko PyongyangPicha: picture-alliance/AP Photo

Mpango wa Korea ya Kaskazini wa silaha zake za nyuklia unaimarika kwa kasi, hadi imefikia sasa kuwepo uwezekano wa Korea ya Kaskazini kuweza kuishambulia Marekani. Rais wa Marekani Donald Trump ameitaka China kutumia uhusiano wake na Pyongyang ili kuwatia moto Korea ya Kaskazini wasimamishe matumizi ya silaha za nyuklia.

Lakini Pyongyang imeendelea na maandalizi yake ya kurusha makombora ya majaribio na hivi sasa wapo katika mpango wa kufanya majaribiao yao ya sita ya makombora.

Mogherini na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa China Yang Jiechi walizungumzia juu ya kuwepo haja ya kushirikiana katika kutafuta suluhu katika migogoro mbalimbali ikiwemo ile ya Syria na Korea ya Kaskazini.

Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence alisema Jumatano wakati akiwa mjini Tokyo alisema kuwa matumizizi yoyote ya silaha za nyuklia kutoka Korea ya kaskazini yatakabiliana na mashambulizi makali na ya nguvu kutoka kwa wanajeshi wa marekani.

Mwandishi: Najma Said

Mhariri:       Iddi Ssessanga