1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo wa Korea Kaskazini

5 Aprili 2013

Hayo yamesemwa na Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry akilaani mpango huo na kusema Marekani ipo tayari na ina uwezo wa kujilinda pamoja na washirika wake dhidi ya silaha hizo za Korea Kasikazini.

https://p.dw.com/p/189xR

Hofu ya Serikali ya Marekani inazidi baada ya Korea Kaskazini kuendelea na utengenezaji wa Silaha za Nyuklia zenye masafa marefu, akiongeza kuwa Marekani inaona kuwa huo ni mpango usiokubalika.

Akiongea katika mkutano wake na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Korea Kusini, Yun Byung-se, Waziri Kerry amesema kuwa licha ya utengenezaji huo wa silaha unaofanywa na Korea Kasikazini, Marekani itaendelea kuishauri Korea Kaskazini kuachana na mpango wake silaha za Nyuklia.

Marekani inaamini kuwa kuna njia rahisi kwa Korea Kasikazini kuitikia wito wa Jumuiya za kimataifa na kukaa katika meza ya mazungumzo ili kutafuta njia rahisi na ya amani ya kumaliza tatizo la Nyuklia kwa kukaa na nchi zingine pamoja na nchi jirani na mshirika wake China.''

Waziri mambo ya nje wa Korea, Mabalozi wa Korea Kusini na Kaskazini pamoja na Waziri wa mambo ya nje wa Merekan hapo jana, walikuwa na mazungumzo magumu kuhusu hali ya wasiwasi iliyopo katika rasi ya Korea Kaskazini.

Akiongea katika mkutano huo waziri wa ulinzi wa China, amesema kuwa serikali ya Marekani na China lazima zishirikiane ili kumaliza tatizo la utengenezaji wa silaha za Nyuklia unaofanywa na Korea Kaskazini.

Hali ya wasiwasi baina Marekani na washirika wake, haijaanza hivi karibuni bali ni ya miongo kadhaa tokea kumalizika kwa vita ya Korea mwaka 1950-1953 lakini hali ya wasiwasi kwa sasa inaonekana kuzidi ikihofiwa kuwa Korea Kaskazini ina mpango wa kukifufua kinu chake cha Nyuklia.

Katika miezi ya hivi karibuni Korea Kaskazini iliitisha Marekani baada ya Korea hiyo kuzindua mpango wake wa kurushia makombora ya nyuklia ya masafa marefu zaidi.

Mwandishi: Hashim Gulana /REUTERS &AP

Mwandishi: Josephat Charo