MZOZO WA GESI: Umoja wa ulaya wadai kuzipatanisha Urusi na Ukraine. | Matukio ya Kisiasa | DW | 09.01.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

MZOZO WA GESI: Umoja wa ulaya wadai kuzipatanisha Urusi na Ukraine.

Mataifa ya ulaya ambayo yameathiriwa na mzozo wa gesi kati ya Urusi na Ukraine yanataraji kuwa hali itarejea kuwa ya kawaida baada ya umoja wa nchi hizo kudai umeweza kuzipatanisha pande zote mbili.

default

Mkurugenzi wa kampuni Gazprom nchini Urusi Alexei Miller, kulia na rais wa bunge la Ulaya Hans-Gert Poettering baada ya kuzungumza na waandishi habari, Brussels.

Hatua hii imetoa afueni kwa walio katika mataifa hayo, kwani kwa sasa ni majira ya baridi kali na watu wa nchi hizo wageathirika kwa kiasi kikubwa

Katika mazungumzo yaliyokamilika usiku wa jana bado hakukuwa na makubaliano yeyote kuhusu Urusi kurejesha huduma zake za kusambaza gesi katika bara la ulaya kupitia mabomba ya ukraine.

Hata hivyo katika tangazo ambalo halikuwa likitarajiwa Czech ambayo ndio rais wa muda wa umoja wa ulaya ilitangaza kuwa waziri mkuu wa Urusi Vladmir Putin alikuwa amekubali kuhusu swala kuu la kupelekwa kwa wasimamizi wa umoja huo kuchunguza usambazaji gesi kupitia ukraine.

Shule kadhaa mashariki mwa bara la ulaya zimefungwa na maelfu ya watu hawana njia ya kuweka vyumba vyao katika hali ya joto, katika kipindi hiki cha msimu wa baridi katika mataifa hayo,kutokana mzozo huo wa mataifa hayo mawili.

Kansela wa ujerumani ni Angela Merkel alipendekeza kupelekwa kwa wasimamizi watakaofuatilia shughuli za usafairishaji gesi kati ya mataifa hayo mawili na pia kutaka kuafikiwa suluhisho la haraka.Ni swala liloungwa mkono na waziri mkuu wa Urussi Vladmir Putin.

Tunakubaliana kabisa na kansella wa ujerumani bi Angela Merkel kuwa wazo langu moja limebuni pendekezo ambalo wachunguzi wa kimataifa watatumwa kwenda kuangalia hali ilivyo katika vituo vya gesi na namna gesi hiyo itakavyopita.Kwa kadri itakavyofanyika haraka ndio itakavyokuwa vizuri „.

Wasimamizi wa umoja ulaya wanaratajiwa kusafiri hadi Ukraine hivi leo, hatua inayoonekana kama swala kuu la kuishinikiza Urusi kurejesha huduma zao za gesi.Hata hivyo hadi sasa hakuna thibitisho kutoka maafisa wa Urusi kuhusu kufanikiwa kupata utatuzi katika mzozo huo.Waziri mkuu wa Urusi Vladmir Putin

“Chakusikitisha ni kuwa lazima tuwe na mazungumzo ya hali ya juu kuhusu ufisadi.Kwangu mimi naona tatizo usimamizi sio kuhusu bei ya gesi, lakini kubadilisha njia tuwe wazi ,faida ipatikane na kutumiwa kwa malengo fulani „.

Mkurugenzi wa kampuni ya gesi ya Urusi Gazprom Alexei Miller aliwaambia waandishi wa habari hapo jana kuwa punde baada ya kutumwa kwa wasimamizi hao, huduma za gesi zitarejeshwa mara moja. Mwenyekiti wa kamati ya mwaswala ya kigeni katika bunge la Urussi Konstantin Kosatschew, alisema haya baada ya mashauri ya Brussels.

Tumepata sura kuwa ujumbe wa Ukraine uliokwenda Brussels haukuwa kabisa huru. Inaonekana kwetu sisi hatua zao zilipatikana na kuathirika kupitia agizo la kisiasa kutoka kiev, ili swala hili liwe la siasa. Kwa muda mrefu ingekuwa wataalam kutoka Urussi na Ukraine kuanzia mwisho wa mwezi december mwaka jana na mapema mwaka huu wagezungumza,basi makubaliano yangeafikiwa kwa haraka. „

Moscow inarataji kuwa mazungumzo kuhusu mzozo huo wa gesi kati ya kampuni ya Urussi ya GazProm na ile ya ukraine Naftogaz yataendelea hivi leo. Kwa mujibu shirika la habari la Itar Tass News hakukuwa na ishara zotote kuwa Mkurugenzi wa kampuni ya Gazprom ALexei Miller na mkurugenzi wa kampuni ya Ukraine, Naftogaz Oleg Dubyna watakutana. • Tarehe 09.01.2009
 • Mwandishi Jane Nyingi
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GV2P
 • Tarehe 09.01.2009
 • Mwandishi Jane Nyingi
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GV2P
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com