1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Myanmarr

14 Novemba 2010

Suu Kyi ameachiliwa huru.

https://p.dw.com/p/Q87e
Kiongozi anayeunga mkono demokrasia Myanmar, Aung San Suu Kyi.Picha: AP

Serikali ya kijeshi ya Myanmarr imemuachilia huru kiongozi anayeunga mkono demokrasia, Aung San Suu Kyi aliyekuwa katika kifungo cha nyumbani.

Aung San Suu Kyi
Wafuasi wa Aung San Suu Kyi washerehekea.Picha: AP

Suu Kyi aliwaambia maelfu ya wafuasi wake waliokusanyika nje ya nyumba yake, kwamba inabidi wafanye kazi kwa umoja ili waweze kufikia malengo yao. Mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel amekuwa kizuizini kwa miaka 15 kutoka 21 iliyopita.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel  amemtaja Suu Kyi kama mtu muhimu katika kupigania  haki za binaadamu duniani.Merkel ameungana na wengine kutoa wito kwa nchi hiyo kuwaachilia huru wafungwa wengine wa kisiasa walio zaidi ya 2000. Nae Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barosso, amesema ni muhimu kwa Suu Kyi kupewa uhuru wa kutembea na kuzungumza bila ya vikwazo vyo vyote.

Mwandishi: Maryam Abdalla/Afpe/Dpae/Rtre

Mhariri:Prema Martin