1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwuaji wa wafanyakazi wawili wa DW nchini Afghanistan akamatwa

Esther Broders / Maja Dreyer20 Agosti 2007

Kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan, alizungumza hasa juu ya matokeo yanayohusiana na kuachiliwa huru mateka mwanamke wa Kijerumani. Lakini pia aliarifu kwamba mtu aliyewaua wafanyakazi wawili wa Deutsche Welle mwaka uliopita amekamatwa. Tangu hapo, jamaa zake, marafiki na wafanya kazi wenziwao hawakujua kabisa nini kimetokea usiku huo wa mauaji.

https://p.dw.com/p/CH9O
Kwa nini mwandishi habari Karen Fischer wa Deutsche Welle ameuawa Afghanistan?
Kwa nini mwandishi habari Karen Fischer wa Deutsche Welle ameuawa Afghanistan?Picha: DW

Bado haijulikani mtuhumiwa aliyekamatwa ni nani na kwa nini aliwaua wafanyakazi wawili wa Deutsche Welle, Karen Fischer na Christian Struwe.

Lakini kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan, Semarai Baschari, kukamatwa kwake siku chache zilizopita ni hatua ya kwanza katika kuchunguza sababu ya mauaji haya: “Miezi kadhaa iliyopita, waandishi hao wawili waliuawa kwenye wilaya ya “Tala-wa Barfak”. Wahalifu hawakujulikana. Kikosi maalum cha polisi kinachoshughulikia vita dhidi ya ugaidi kilianza uchunguzi wakati huo. Wiki iliyopita kimeweza kumkamata kiongozi wa kundi dogo la wahalifu ambalo lilihusika katika mauaji hao. Hivi sasa, uchunguzi unaendelea na tunajaribu kuwakamata wahalifu wengine wa kundi hilo.”

Msemaji huyu wa wizara ya ndani hakutaka kusema zaidi juu ya sababu ya kutokea mauaji haya: “Hatujui kwa hakika, kwa nini kundi hili limefanya kitendo hicho. Aliyekamatwa yu mikononi mwa polisi mjini Kabul na uchunguzi unaendelea.”

Serikali ya Ujerumani haikuthibitisha habari hizo. Wafanyakazi hao wawili walipigwa risasi mwezi wa Oktober mwaka jana wakiwa Kaskazini mwa Afghanistan. Wahalifu waliwashtukizia usiku kwenye hema lao karibu kwenye kijiji kimoja karibu na barabara. Mtuhumiwa alikamatwa katika wilaya hiyo hiyo ambapo mauaji yalitokea. Kulingana na msemaji wa serikali Semarai Basch

ari, kesi hiyo haina uhusiano wowote na utekaji nyara wa mwanamke mwingine wa Kijerumani ambaye aliachiliwa huru jana. Semarai Baschari alisema: “Matukio haya mawili hayana maingiliano. Ni kwa bahati tu kwamba tumetoa habari juu ya yote mawili.”

Waandishi habari Karen Fischer na Christian Struwe walifanya kazi kwenye Deutsche Welle kwa muda. Wote wawili walilitembelea nchi za kigeni kwa azma ya kufanya kazi yao ya uandishi habari, hususan nchini Afghanistan. Christian Struwe alisaidia katika ujenzi mpya wa ofisi ya televisheni ya kiserikali inayoshughulikia habari za kimataifa. Bi Karen Fischer alikuwa mwandishi wa Redio Deutsche Welle naye alisafiri kwenda Afghanistan mara kwa mara kutayarisha ripoti juu ya matokeo muhimu kama vile uchaguzi wa mwaka 2005.