1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwongozo wa sera za Ujerumani kuelekea Afrika

23 Mei 2014

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amelimwagia sifa bara la Afrika na kusema bara la Afrika linakaribia kuwa " bara lenye fursa" imeeleza wizara ya mambo ya kigeni.

https://p.dw.com/p/1C4zr
Angela Merkel 2014 ernste Mimik
Kansela wa Ujerumani Angela MerkelPicha: picture-alliance/dpa

Vyombo vya habari, ambavyo huvutiwa kwa kiasi kikubwa na habari za kuzama kwa maboti, utekaji nyara na mauaji, hufuatilia pia taarifa za sera za maendeleo na matumizi ya jeshi. Ni mara chache imeoneshwa Afrika halisi. Lakini katika siku za hivi karibuni , hajajitokeza fursa , bali kitisho na hali ile ile ya kuliona bara hilo kama lilivyokuwa linaelezwa nchini Ujerumani hapo zamani.

Nigeria, Jamhuri ya Afrika ya kati, Sudan kusini, Mali. Katika kutangazwa kwa mtazamo mpya wa serikali ya Ujerumani kuelekea bara la Afrika, anaeleza msemaji wa serikali ya Ujerumani Steffen Seibert, kwamba maeneo yenye matatizo katika bara hilo ,maafa, vita yanajitokeza kila mara. Ukuaji imara wa kiuchumi katika mataifa kadha ya Afrika mara nyingi hauangaliwi.

Mataifa ya Afrika yawajibike

Mwongozo wa sera ya bara la Afrika ya serikali ya Ujerumani inaangalia yote hayo kwa pamoja, anasema Seibert. Mwongozo huo ambao ulikubaliwa siku ya Jumatano tarehe 21.05.2014 unalenga zaidi katika wajibu wa mataifa ya Afrika, utawala bora na kufuata sheria, demokrasia na elimu, na hayo pia si mageni, badala yake ni muendelezo zaidi wa sera zilizokuwapo.

Dr. Gerd Müller
Dr. Gerd MüllerPicha: Bundesregierung Kugler

Uchumi endelevu wa masoko unaoweza kutumiwa na sehemu kubwa ya wananchi , ni suala ambalo limezungumziwa na serikali zilizopita. Majadiliano ya kina, kufanyakazi kwa ushirikiano katika kiwango sawa, ushirikiano na mataifa ya Afrika katika changamoto za dunia, huu ni msisitizo mpya unaowezekana.

Katika siku za nyuma Waafrika walikuwa wakitupwa kando katika masuala ya kanuni, na utaratibu. Katika suala la nafasi za uongozi katika mashirika kama benki kuu ya dunia na shirika la fedha la kimataifa , katika tathimini ya kundi la mataifa yanayoinukia na yaliyoendelea duniani G20 ama kwa mtazamo wao wanapewa masharti ambayo si ya haki na Umoja wa ulaya inapokuja katika mikataba ya ushirikiano katika masuala ya kiuchumi.

Chama cha Ujerumani cha masuala ya uchumi kwa bara la Afrika , ambacho kina makampuni 600, kinaona katika muongozo huu , ishara nzuri. Serikali ya Ujerumani inatambua , kwamba bara la Afrika limebadilika. Hususan chama hicho cha masuala ya uchumi kinafarijika , kwamba wawekezaji katika bara la Afrika wakiwa kile kinachojulikana kama garantii ya kulipa madeni inayotolewa na Hermes ni nzuri kwa kulinda athari yoyote itakayotokea, suala ambalo ni moja kati ya mambo ambayo yanadaiwa na chama hicho.

Wapinzani wapuuzia

Kwa upande wa upinzani mwongozo huo kuhusu Afrika haukupata upendeleo wa kutosha. Msemaji wa sera ya maendeleo wa chama cha walinzi wa mazingira , Uwe Kekeritz, ameikosoa, na kusema ni maneno matupu , na maneno ya kutia moyo tu. Mwongozo huo kwa kiasi kikubwa haukulenga popote, amesema Kekeritz. Hakuna hatua za maana zilizopangwa, kwa hiyo ni vipi litaweza kufikiwa lengo. Kimsingi mwongozo huo hauna maana. Kwa njia moja ama nyingine katika siku zilizopita mwongozo kama huo kwa ajili ya Afrika ama mpango kwa ajili ya Afrika ulikuwapo.

Hali hiyo haitusaidii kusonga mbele kimsingi. Amesema msemaji huyo wa chama cha walinzi wa mazingira.

Jan van Aken DIE LINKE Porträt
Msemaji wa Die Linke Jan van AkenPicha: picture-alliance/dpa

Mtaalamu wa masuala ya mambo ya kigeni wa chama cha Die Linke , Jan van Aken , ameonya dhidi ya kupeleka majeshi ya Ujerumani nchi za nje. Katika mwongozo kuhusu bara la Afrika upelekaji wa vikosi vya jeshi la Ujerumani si kitu kinachoweza kuepukwa. Chama cha Die Linke kina shaka na jeshi kuwa ni sehemu ya sera za mambo ya kigeni. Serikali ya Ujerumani itakuwa inachokoza hali ya ghasia katika bara la Afrika na katika kanuni hii ni sawa tu, anasema van Aken katika mazungumzo na DW. " Ni katika wakati tu , ambapo maslahi ya Ujerumani ama Ufaransa yameguswa, ndipo kutakuwa na umuhimu.

Mwandishi : Claus Stäcker / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri: Josephat Charo