1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwito kutekeleza Malengo ya Milenia

27 Januari 2008

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametoa mwito kwa viongozi wa kimataifa kukubaliana kuhusu baadhi ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia yanayotazamiwa kutimizwa ifikapo mwaka 2015.

https://p.dw.com/p/CyUP
Secretary-General of the United Nations Ban Ki-moon speaks during a media conference at the World Economic Forum in Davos, Switzerland, Friday Jan. 25, 2008. Buoyed by a burst of optimism from Bill Gates, business and government leaders attending the World Economic Forum were set Friday to hear more about positive things they can do after two days of confronting fears. (AP Photo/Peter Dejong)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon akizungumza katika Mkutano wa Uchumi Duniani mjini Davos,UswisiPicha: AP

Ban Ki Moon akizungumza katika kikao maalum kilichoitishwa pembezoni mwa Mkutano wa Uchumi Duniani katika mji wa Davos nchini Uswisi,amewataka viongozi wa kimataifa wakubaliane kutimiza baadhi ya malengo ya mwaka 2015 ifikapo mwaka 2010.Kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown,Rais wa Nigeria Umaru YarÁdua,Malkia Ranai wa Jordan pamoja na muasisi wa kampuni ya Microsoft-Bill Gates na mwana muziki mashuhuri Bono.

Katibu Mkuu Ban amekumbusha kuwa hadi sasa maendeleo yaliyopatikana ni asilimi 30 tu ya vile ilivyopangwa.Amesema bila ya jitahada zaidi,itakuwa shida kuyatimiza Malengo ya Mandeleo ya Milenia.Malengo hayo yalipangwa mwanzoni mwa milenia hii katika mwaka 2000 kwa matarajio kuwa mafanikio yatapatikana katika sekta nyingi.

Miongoni mwa malengo yanayotazamiwa kutimizwa kabla ya mwaka 2015 ni kuondosha umasikini miongoni mwa watu milioni 75 barani Afrika,kuwapatia elimu ya msingi zaidi ya watoto milioni 25 pamoja na kuokoa maisha ya watoto wapatao milioni 4 kwa kuongeza idadi ya wasaidizi wanaohudumia akina mama wakati wa uzazi ili kupunguza kwa theluthi mbili vifo vya watoto wachanga na mama wazazi pamoja na kupambana na magonjwa kama UKIMWI na malaria bila ya kuwasahau watu milioni 70 wanaohitaji kupatiwa maji ya kunywa.Kwa jumla ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2020, kutapatikana maendeleo yatakayoboresha hali za walala hoi wapatao kama milioni 100 na wakati huo huo kutakuwepo ushirikiano wa kimataifa kuleta maendeleo.

Ban ki-Moon amesema,ulimwengu unapaswa kujitolea upya mwaka huu wa 2008 kushughulikia matatizo yanayowakabili mamilioni ya watu wanaoishi kwa kutumia chini ya Dola moja kwa siku.Mwanaharakati Bono anaeongoza kampeni ya kusaidia nchi masikini barani Afrika,amewalumu viongozi wa serikali na mashirika makuu ya kibiashara duniani kuwa hawakutekeleza Malengo ya Milenia yaliyokubaliwa.Amesema wakati ndio umewadia kuchukua hatua kuhusu Malengo yaliyopangwa.

Lakini Kumi Naidoo alie Katibu Mkuu wa kundi la kijamii linaloongoza juhudi za kupiga vita umasikini duniani,amesikitika kuwa masuala yanayohusika na umasikini hayapati kipaumbele kama ule mzozo wa kifedha na soko la benki uliotawala Mkutano wa Uchumi mwaka huu mjini Davos.