Mwito kujiunga na Al-Qaeda Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 06.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Mwito kujiunga na Al-Qaeda Afghanistan

DUBAI:

Kiongozi wa kundi la al-Qaeda nchini Afghanistan amewahimiza Waislamu zaidi kujiunga na kundi hilo kupigana vita nchini humo.Mustafa Abu al-Yazid katika tovuti ya wanamgambo wa Kiislamu ameomba msaada wa fedha pia na amesema,majeshi ya Magharibi nchini Afghanistan yanakaribia kushindwa.

Vikosi vya Marekani na vya Jumuiya ya Kujihami ya Magharibi NATO vinapambana vikali na wanamgambo waTaliban na makundi ya al-Qaeda nchini Afghanistan.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com