Mwishoni mwa wiki hii | Michezo | DW | 16.11.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Mwishoni mwa wiki hii

Brazil yarudi uwanjani kuumana na Peru kwa tiketi ya kombe la dunia 2010.Comoro na Madagascar zaumana Moroni na kanda Ulaya ,Ujerumani ina miadi na cyprus kuania tiketi ya Euro 2008.

default

Lukas Podolski

Kocha wa zamani wa simba wa nyika-kameroun,Winfried Schäfer kuwa kocha wa timu ya taifa ya Iran ? Bayern Munich kutumia dala milioni 20.45 kwa chipukizi wa Sao Paulo ya Brazil,Breno.

Brazil leo ina miadi na peru katika kinyan’ganyiro cha kanda ya Amerika kusini cha kuania tiketi za finali ya kombe la dunia 2010.

Abedi Pele akiwa Uganda,apendekeza kuasisiwa kwa Chu o cha dimba kwa chipukizi-soccer Acadamy.

Tuanze na kinyan’ganyiro cha kan da ya Amerika kusini cha kuania tiketi za Kombe lijalo la dunia.

Baada ya leo Comoro na Madagascar kurudi uwanjani kwa duru ya pili mjini Moroni kuania tiketi zao za kombe la dunia 2010,mabingwa mara 5 wa dunia-Brazil watazamia nao kesho kutamba mbele ya Peru kanda

Katika mapambano 2 ya kwanza ya kinyan’ganyiro hiki, Peru haikuona mlango hata mara moja lakini ushindi kesho dhidi ya Brazil nyumbani Lima, utawafutia madhambi yaliopita na kuwafungulia njia mpya ya kwenda Afrika Kusini.Peru inateremka kesho uwanjani ikiwa na pointi 1 tu wakati Brazil wana pointi 4 baada ya kuirarua Ecuador kwa mabao 5:0 hivi majuzi.

Kuna shaka shaka iwapo kocha Dunga atamteremsha kesho Ronaldinho, anaechechemea.Hatahivyo, goti lake halijambo kidogo.Ronaldinho alifanya mazowezi kidogo juzi alhamisi lakini baadae aliondoka uwanjani.

Taarifa kutoka Berlin mwishoni mwa wiki hii zinaarifu kwamba, aliekua kocha wa timu ya taifa ya kameroun-simba wa nyika Winfried Schäfer anazungumza kuwa kocha wa timu ya taifa ya Iran-hii ni kwa muujibu wa gazeti la DIE WELT la Ujerumani.Mazungumzona viongozi wa dimba wa Iran yatakuwa jumatatu nchini Ujerumani.

Schäfer akasema kwamba kazi hiyo inamvutia na kwamba timu ya Iran ni kali.Anawajua baadhi ya wachezaji kama vile Ali Karimi.Iran inazeeka kidogo na haikutamba karibuni katika Kombe la Asaia.hatahivyo, alisema Schäfer,ina chipukizi wengi mastadi.Iran inasimama ngazi ya 38 katika orodha ya FIFA.

Mjini Accra,kituo cha kombe lijalo la afrika la mataifa januari mwakani, kesho itachezwa nusu-finali ya mashindano ya mataifa 4.Wenyeji – Ghana wana miadi na Umoja wa Falme za kiarabu (Emirates.)

Viongozi wa Ligi ya ujerumani-Bundesliga-Bayern munich wanapanga kumuajiri chipukizi wa Brazil.mlinzi wa Sao Paulo Breno.Munich iko tayari kutumia kitita cha dala milioni 20.45 kwa ajili ya Breno mwenye umri wa miaka 18 tu.

Aliempendekeza Breno kwa bayern munich ni mshambulizi wao wa zamani Giovanne Elber.Akiwasili munich Breno atajiunga na wabrazil wenzake wanaosakata dimba na Bayern Munich Lucio na Ze Roberto.Hata Real M adrid ikimdowea Breno nah ii ndio ilioifanya Munich kupandisha bei.Munich,imekwishatumia kitita cha Euro milioni 70 mwaka huu kuwaajiri akina Franck Ribery wa Ufaransa,Luca Toni kutoka Itali na Miroslav Klose kutoka Werder Bremen. Sasa inaimarisha ulinzi.

Abedi Pele, mchezaji bora kabisa wa dimba wa mwaka wa Afrika na nahodha wa Black Stars Ghana,alikuwa Kampala , Uganda hivi majuzi.Akiwa huko alitoa nasaha juu ya jinsi ya kuendeleza vipaji vya chipukizi nchini Uganda : Pele alipendekeza kuanzshwe chuo cha dimba kwa chipukizi-Football Acadamy kama ilivyo desturi hivi sasa huko Afrika magharibi.

 • Tarehe 16.11.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CImg
 • Tarehe 16.11.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CImg
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com