Mwili wa mwanamke aliyebakwa kurejeshwa India | NRS-Import | DW | 29.12.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

NRS-Import

Mwili wa mwanamke aliyebakwa kurejeshwa India

Mwili wa mwanamke wa India ambaye amefariki hospitalini nchini Singapore baada ya kubakwa kinyama mjini New Delhi utarejeshwa kwa ndege maalum ya kukodi baadaye leo Jumamosi(29.12.2012).

epa03519152 Indian protesters and commuters light candles during a protest campaign by Youth Congress against the gang rape of a student last week, in Calcutta, India, 28 December 2012. The 23-year-old Indian gang rape victim being treated in a Singapore hospital was in extremely critical condition and struggling to survive, doctors said on 28 December. The woman was raped and beaten in a moving bus in New Delhi on 16 December. The attack triggered protests in the Indian capital and other cities. EPA/PIYAL ADHIKARY +++(c) dpa - Bildfunk+++

Waombolezaji wakiweka mishumaa

Balozi wa India nchini Singapore T.C.A Raghavan amewaambia waandishi habari, saa kadha baada ya mwanamke huko kufariki kutokana na viungo vyake kushindwa kufanya kazi katika hospitali nchini Singapore ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

Mwanamke huyo na ndugu wa marehemu watasafirishwa kwenda India katika ndege maalum ya kukodi baadaye mchana wa leo Jumamosi, (29.12.2012) , amesema Raghavan.

Waziri mkuu ahuzunika

Waziri mkuu wa india Manmohan Singh amesema kuwa amesikitishwa sana na kifo cha mwanamke huyo ambaye alifanyiwa vitendo vya kinyama kwa kubakwa na kundi la vijana na kwamba maandamano yaliyozuka kutoka na kitendo hicho , "yanaeleweka".

epa03518670 An Indian protester holds a candle and others placards, during a silent protest march held by sex workers, transgender and gays, against the gang rape of a student in New Delhi a week back, in Mumbai, India, 27 December 2012. The 23 year old woman who was gang-raped by 6 men on a moving bus on the night of 16 December 2012 has been flown to a Singapore hospital for further treatment of her severe internal injuries. EPA/DIVYAKANT SOLANKI

Wanawake wakiandamana nchini India wakipinga matumizi ya nguvu katika ngono

"nimesikitishwa mno kufahamu kuwa mhanga huyo wa mashambulizi ya kinyama ambayo yalifanyika Desemba 16 mjini New Delhi ameshindwa kunusurika kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata baada ya shambulio dhidi yake, " ameandika waziri huyo mkuu katika tovuti yake.

"Tumekwisha ona hisia na nguvu ambazo tukio hili limesababisha. Hii ni hali ambayo inaeleweka kutoka kwa vijana wa india ambao wanataka mabadiliko ya kweli.

"Nataka kuwaambia , familia yake na taifa kwa jumla kuwa amepoteza maisha, ni juu yetu wote kuhakikisha kuwa kifo chake hakitakuwa cha bure."

Indian Prime Minister Manmohan Singh attends a Full Planning Commission meeting at his residence in New Delhi on September 15, 2012. Indian Prime Minister Manmohan Singh defended September 15 a string of economic reforms unveiled by his government, despite protests over higher fuel prices and new foreign investment rules. AFP PHOTO/POOL/RAVEENDRAN (Photo credit should read RAVEENDRAN/AFP/GettyImages)

Waziri mkuu wa India Manmohan Singh

India imetikiswa na maandamano makubwa tangu msichana huyo mwenye umri wa miaka 23 kushambuliwa kinyama katika basi mjini New Delhi na kundi la watu sita.

Serikali imekuwa ikijaribu kulituliza wimbi la hasira kwa kuahidi adhabu kali kwa uhalifu mkubwa unaohusiana na ngono pamoja na kuunda tume maalum ya uchunguzi kuhusiana na jinsi ya kushughulikia kesi za ubakaji.

Polisi wautaka umma kuomboleza kwa amani

Wakati maafisa wakijitayarisha kwa ghasia zaidi mitaani, polisi wameonekana kuongezwa katika eneo la kati la mji mkuu wa india kabla ya mwili wa msichana huyo mwenye umri wa miaka 23 haujarejeshwa nchini humo. Afisa wa polisi wa mjini New Delhi amehimiza watu kuomboleza kifo cha mwanamke huyo kwa amani wakati maeneo kadha ya mji huo mkuu yamefungwa.

Police detain a demonstrator in front of the India Gate during a protest in New Delhi December 23, 2012. The Indian government moved on Sunday to stamp out protests that have swelled in New Delhi since the gang-rape of a young woman, banning gatherings of more than five people, but still thousands poured into the heart of the capital to vent their anger. REUTERS/Adnan Abidi (INDIA - Tags: CRIME LAW CIVIL UNREST TPX IMAGES OF THE DAY)

Polisi wanajiandaa kwa maandamano makubwa zaidi nchini India

Singh , ambaye hapo kabla alitoa wito wa utulivu , amesema kuwa itakuwa , "Heshima kubwa kwa kumbukumbu yake iwapo tutaweza kuelekeza hisia zetu hizi na nguvu katika kuchukua hatua sahihi."

"Kwa muda huu tunahitaji mjadala wa maana na uchunguzi kuhusiana na mabadiliko ya lazima na haraka ambayo yanahitajika katika mtazamo wa jamii.

"Ni matumaini yangu kuwa tabaka lote la kisiasa pamoja na jamii yote itatenga maslahi yao finyu ya binafsi na ajenda ili kutusaidia kufikia hatima ambayo tunaikusudia, na kuifanya india kuwa mahali bora na salama kwa wanawake kuweza kuishi.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Abdu Mtullya

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com