1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwenyekiti wa SPD akaribisha kuchaguliwa kwake

19 Oktoba 2008
https://p.dw.com/p/Fd0v

Berlin:

Mwenyekiti mpya wa chama cha Social Democrats-SPD nchini Ujerumani Franz Müntefering, ameyakaribisha matokeo ya mkutano mkuu wa chama hicho jana. Wabunge walimuidhinisha Bw Müntefering kuwa Mwenyekiti mpya kwa asili mia 85 ya kura na kumuidhinisha pia Waziri wa mambo ya nchi za nje na Makamu wa Kansela, Frank Walter-Steinmeir kuwa mgombea wa kiti cha Ukansela wa SPD katika uchaguzi mkuu mwaka ujao. SPD ambacho ni mshirika katika serikali ya muungano ya Shirikisho na Christian Democrats-CDU, kina matumaini uongozi mpya wa wanasiasa hao wawili utabadili hali ya hivi sasa ya kupoteza umaarufu,ikiwa ni kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni ya wapiga kura.