1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwenyekiti wa ECOWAS asema mapinduzi ya Mali yanaambukiza

Iddi Ssessanga
3 Februari 2022

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS), rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, amesema mapinduzi ya kijeshi Mali yalikuwa yanaambukiza na yamechochea mapinduzi mengine katika kanda.

https://p.dw.com/p/46TLg
ECOWAS Westafrikanische Staaten verhängen Sanktionen gegen Mali und Guinea
Picha: Nipah Dennis/AFP

Rais Nana Akufo-Addo ametoa kauli hiyo katika mkutano wa kilele wa wakuu wa mataifa ya kanda hiyo, kujadili mapinduzi ya kijeshi nchini Burkina Gaso, na vitisho vinavyoibuka katika kanda hiyo vilivyoanza na uingiliaji wa kijeshi nchini Mali na ushawishi wake wa kuambukiza nchini Guinea na Burkina Faso.

Mwenyekiti huyo wa ECOWAS amesema muekeleo huo laazima udhibitiwe kabla ya kuiharibu kanda nzima.

soma zaidi: Mali yampa balozi wa Ufaransa saa 72 kuondoka nchini humo

Mapinduzi ya Agosti 2020 nchini Mali yalifuatiwa na mapinduzi ya pili nchini humo Mei mwaka jana, nchini Guinea mwezi Septemba mwaka jana, mapinduzi ya kijeshi wiki iliyopita nchini Burkina Faso, na mapinduzi yalioshindwa Guinea-Bissau siku ya Jumanne.