1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanasiasa mashuhuri Hassan Nassor Moyo afariki dunia

Iddi Ssessanga
18 Agosti 2020

Mwanasiasa mkongwe Visiwani Zanzibar ambaye aliwahi kushikilia nafasi mbalimbali kwenye serikali ya Zanzibar na ile ya Muungano wa Tanzania, Mzee Hassan Nassor Moyo, ameaga dunia.

https://p.dw.com/p/3h7c5
Tansania Präsidentschaftswahl Mzee Hassan Nassor Moyo
Picha: DW/M. Khelef

Mzee Moyo atakumbukwa kwa mengi, ikiwemo kuongoza wafanyakazi wa Zanzibar kwenye mapambano ya ukombozi wa visiwa hivyo katika siku za ujana wake.

Soma pia Moyo afafanua kilichotokea uchaguzi wa Zanzibar 2010

Moyo alikuwa waziri wa kwanza wa sheria kwenye serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia na pia alikuwa muasisi wa muungano na alikuwa mwenyekiti wa kamati ya maridhiano Zanzibar ambayo baadae yalichangia kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Mzee Nassor Hassan Moyo Interview Politik Sansibar
Mzee Hassan Nassor Moyo akihojiwa na mwandishi wa DW Zanzibar, Salma Said, enzi za uhai wake.Picha: DW/S.Said

Aprili 19, 2015 halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Unguja Magharibi, visiwani Zanzibar, ilkifikia uamuzi w akumvua uanachama wa chama hicho Mzee Moyo, kwa tuhuma za kuchochea kujitenga kwa Zanzibar na mambo mengine.

Soma pia Moyo: Mansoor hakutendewa haki

Licha ya kufukuzwa na chama hicho tawala, Mzee Moyo hakuhamia chama chengine, lakini alikuwa akisisitiza kwamba anamuunga mkono yeyote anayepigania mamlaka zaidi kwa visiwa hivyo ndani ya Muungano wa Tanzania.