Mwanasheria mkuu wa Marekani matatani | Matukio ya Kisiasa | DW | 02.03.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mwanasheria mkuu wa Marekani matatani

Rais wa Marekani Donald Trump ameingia tena katika msukosuko mwengine wa kisiasa  baada ya kubainika Mwanasheria mkuu Jeff Sessions  kudaiwa kufanya mazungumzo na balozi wa Urusi nchini Marekani wakati wa kampeni.

USA Proteste bei der Anhörungen von Trumps Kabinettskandidaten Jeff Sessions (picture-alliance/R. Sachs/CNP/MediaPunch)

Mwanasheria mkuu wa Marekani Jeff Sessions aliengia matatani kwa kuwasiliana na Urusi

Mawasiliano hayo yamezusha wito katika bunge la Marekani la kumtaka kujiondoa katika uchunguzi unaofanywa na wizara ya sheria juu ya Urusi kuuingilia uchaguzi wa Marekani ulimwingiza madarakani Trump.

Sessions, ambae ni muungaji mkono wa mwanzo kabisa wa Rais Donald Trump na mshauri wa kisera wa mgombea wa chama cha Republican, hakuwaweka wazi kile walichozungumza na balozi huyo wa Urusi wakati shauri hilo liliposikilizwa  mwezi uliopita pale alipoulizwa atafanya nini pale yeyote akibainika katika kampeni ana mawasiliano na maafisa wa Urusi. Mwanasheria huyo mkuu alijibu hajafanya mawasiliano na Warusi.

Jumatano usiku msemaji wa wizara ya sheria Sarah Isgur Flores alisema alisema kwa hakika hakuna kilichopotoshwa katika majibu yake hayo. Taarifa hiyo haikukidhi matakwa ya Wademokrat, ambao kabla ya siku hiyo walishinikiza kiongozi huyo ajiondoe katika muendelezo wa uchunguzi na kuzusha maswali ya uwezekano wa kusimamia vyema uchunguzi.

Kauli ya kiogozi wa upinzani bungeni

Nancy Pelosi (Getty Images/W. McNamee)

Kiongozi wa wabunge wa chama cha Demokratik Nancy Pelosi

Kiongozi wa chama cha Demokratik katika bunge la Marekani Nancy Pelosi amemtuhumu Sessions kwa kuongopa pamoja na kula kiapo na akataka ajiuzulu. Wademokratik wengine wamepiga kelele za kutaka ajiweka kandoni na uchunguzi huo. 

Katika taarifa yake Ijumaa jioni, Sessions alisema hajawahi kukutana na afisa yeyote wa Urusi kujadili suala la kampeni. Hana fikra zozote kuhusu tuhuma hizo. Na kuongeza kuwa ni upotoshaji. Lakini kitengo cha uchugzi kimethibitisha kuwa, akiwa kama Seneta wa Marekani na mwanachama mwandamizi wa kamati ya bunge ya huduma za silaha, mwanasheria huyo mkuu anatajwa kufanya zaidi ya majadiliano 25 na mwaka jana, na amefanya mazungumzo mengine mara mbili tofauti na balozi wa Urusi Sergey Kislyak.

Moja katika mikutano hiyo ulifanyika Septemba akiwa Seneta, sambamba na mikutano mingine na wajumbe wa Uingereza, Chuina, Ujerumani na mataifa mengine. Mwengine ulifanyika kwa makundi baada ya hotuba ya hafla maalumu ya Wakfu wa Urithi, ambayo mtuhumuwa aliitoa katika kipindi cha kiangazi. Hafla hiyo ilijumuisha mabalozi kadhaa akiwemo wa Urusi. Balozi huyo anatajwa alikwenda moja kwa Sessions baada ya kuzungumza wakati anaondoka katika jukwaa. Habari hizo za mawasiliano, kwanza kabisa  ziliandikwa na gazeti la Washington Post.

Mwabdishi: Sudi Mnette APE

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

 

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com