1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanamke dereva wa lori la taka Mombasa

Fathiya Omar5 Agosti 2020

Makala ya Wanawake na Maendeleo leo inamuangazia mwanamke mmoja dereva wa lori la taka mjini Mombasa maarufu kama Mama Chiku Mohammed. Utasikia changamoto katika kazi yake na pia mafanikio aliyopata kutokana na kazi hiyo. Nahodha wako ni Fathiya Omar.

https://p.dw.com/p/3gPbP

Anapokuwa barabarani Chiku yuko ngangari kweli kweli anapopambana na msongamano wa magari. Anahakikisha kuelekea katika kila kona ya sehemu aliyopangiwa kukusanya taka. Analiegesha gari kando na wenzake wanashuka kuokota takataka zilizotupwa pembezoni mwa barabara.

Kenia Dandora Mülldeponie in Nairobi
Picha: DW/J. Charo

Kwa miaka yote, magari haya yamekuwa yakihudumiwa na wanaume. Lakini mama Chiku amevunja rekodi hiyo kwa kuwa dereva wa kwanza mwanamke kuendesha lori la kubebea taka katika kaunti ya Mombasa.