Mwanamfalme Harry amerudi Uingereza | Habari za Ulimwengu | DW | 01.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mwanamfalme Harry amerudi Uingereza

LONDON:

Mwanamfalme Harry amerejea Uingereza kutoka Afghanistan baada ya kuwepo huko kwa siri pamoja na majeshi ya Uingereza.Harry,alie na cheo cha luteni wa pili jeshini alikuwepo Afghanistan kwa majuma 10 pamoja na kikosi cha Uingereza kinachopambana na Wataliban katika wilaya ya Helmand,kusini mwa nchi. Mwanamafalme Harry mwenye umri wa miaka 23 alitazamia kubakia Afghanistan pamoja na wanajeshi wenzake hadi mwezi wa Aprili.Lakini Wizara ya Ulinzi ya Uingereza,imeamua kumrejesha nyumbani baada ya vyombo vya habari vya kigeni kufichua kuwa yupo Afghanistan.

l

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com