1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanaharakati wa CCM atishiwa kufukuzwa kutoka chamani

11 Septemba 2008

Nchini Tanzania mwenyekiti wa chama tawala cha Mapinduzi CCM amempa mwanasiasa Nape Nnauye ruhusa ya kukata rufaa iwapo anaona hakuridhika na uamuzi wa kumvua uanachama wa Umoja wa Vijana wa chama hicho, UVCCM.

https://p.dw.com/p/FG62
Rais J.K.Kikwete alitoa taarifa fupi kwenye kikao cha NEC kuhusu Nape NauyePicha: AP Photo

Hatua hiyo inatofautiana na katibu wake, Yusuf Makamba, ambaye alisema kijana huyo hawezi kukata rufaa katika chombo chochote.Rais Kikwete, akitoa taarifa fupi kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) jana, pia alisema chama hicho tawala kitaendelea kumtambua Nape kama mjumbe wake, mwanachama na kutambua nyadhifa zake zote ndani ya CCM.Kauli hiyo ni kinyume mapendekezo ya Baraza Kuu la UVCCM lililotaka mwanasiasa huyo avuliwe nyadhifa zake zote.Mvutano huo unaashiria nini katika chama tawala? Hilo ndilo suali Thelma Mwadzaya alilomuuliza Prof Baregu Mwesiga mhadhiri wa uhusiano wa kimataifa na siasa katika chuo kikuu cha Dar es salaam nchini Tanzania