1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanaanga wa mwisho kutembea mwezini afariki dunia

Sylvia Mwehozi
17 Januari 2017

Eugene Ceman, Mmarekani na Mwanaanga wa mwisho kutembea mwezini amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.

https://p.dw.com/p/2VuYj
Gene Cernan ehemaliger Astronaut
Picha: Getty Images/AFP

Eugene Ceman, Mmarekani na Mwanaanga wa mwisho kutembea mwezini amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.

Cerman alikuwa ni kamanda wa chombo cha anga cha Apollo 17 na ujumbe wake uliwasili mwezini mwaka 1972.

Kwa mujibu wa tangazo la familia yake lililotolewa na Shirika la anga za juu la Marekani NASA mwanaanga huyo mstaafu alifariki kutokana na matatizo ya kiafya.

"Hata katika umri wa miaka 82, Gene alikuwa na mapenzi ya kuona binadamu wanaendelea kwenda mwezini na kuwahamasisha viongozi wa kitaifa na kizazi kipya kuhakikisha kwamba yeye hatokuwa mtu wa mwisho kutembea mwezini" ilisema taarifa hiyo.

Cerman alitumia muda wa masaa 566 na dakika 15 katika anga, na kutumia masaa zaidi ya 73 mwezini.

Mwandishi: Sylvia Mwehozi/AFP

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman