1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwalimu wa Uingereza afungwa siku 15 nchini Sudan

30 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CV84

Serikali ya Uingereza imesema itajitahidi kupata uhuru wa mwalimu wa Kingereza alieadhibiwa nchini Sudan,kifungo cha siku 15 kwa mashtaka kuwa aliitusi dini ya Kiislamu alipowaruhusu wanafunzi wake kumpa dubu la sanamu yaani „teddy bear“ jina la Mohamed.Balozi wa Sudan mjini London ameitwa katika ofisi ya Waziri wa Masuala ya Nje wa Uingereza Miliband.

Mwalimu Gillian Gibbons mwenye umri wa miaka 54 hajakutikana na hatia ya kudharau imani za kidini,ama sivyo angekabiliwa na kifungo cha mwaka mmoja,kupigwa viboko 40 au kutozwa faini. Makundi ya Waislamu wa nchini Uingereza yamelaani hukumu ya mahakama ya Sudan na hatua ya hata kuifikisha kesi hiyo mahakamani.