Mwalimu Gibbons amesemehewa na Rais wa Sudan | Habari za Ulimwengu | DW | 04.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mwalimu Gibbons amesemehewa na Rais wa Sudan

Mwalimu wa Kingereza Gillian Gibbons aliekuwa jela siku 9 nchini Sudan amesharejea Uingereza baada ya kusamehewa na Rais wa Sudan Omar Hassan el-Bashir.Mwalimu Gibbons alipewa kifungo cha siku 15 kwa mashtaka kuwa aliitusi dini ya kiislamu alipowaruhusu wanafunzi wake kutumia jina la Mohamed kwa dubu la sanamu yaani teddy bear.Gibbons alisamehewa siku ya Jumatatu,baada ya wabunge wawili wa Kiislamu wa Uingereza kwenda Khartoum kuomba aachiliwe huru.Juma lililopita, maelfu ya watu waliandamana katika mji mkuu wa Sudan na kudai kuwa mwalimu huyo apewe adhabu ya kifo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com